Tunaalika shirika lako kuwasilisha uteuzi kwa Awamu ya 2024 ya (toleo la tisa) Stevie® Awards kwa Waajiri Bora (Stevie® Awards for Great Employers), tuzo kuu duniani kwa mafanikio ya wafanyakazi, timu, na wataalamu, na bidhaa na huduma mpya, na wauzaji, ambao husaidia kuhakikisha na kuendesha mazingira bora ya kazi.
Ikiwa ungependa kupokea zana ya kuingia, ikiwa na maagizo kamilifu kuhusu jinsi ya kuandaa na kuwasilisha uteuzi wako, wasilisha anwani yako ya barua pepe hapa na tutakutumia barua pepe. Tuna sera kali ya faragha na hatutashiriki anwani yako ya barua pepe kwa mtu mwingine yeyote, kwa sababu yoyote.
Huu ndio ukurasa pekee kwenye tovuti hii ambao utauona katika lugha hii. Kurasa zingine zote ziko katika Kiingereza, kama vile zana ya kuingia. Hii ni kwa sababu tunahitaji ombi la uteuzi liwasilishwe kwa Kiingereza, ili wataalamu wa biashara duniani kote waweze kushiriki katika mchakato wa kuamua. Ifuatayo ni muhtasari mfupi wa tuzo, mahitaji ya uwasilishaji, na faida za kushiriki. Ukiamua kwamba shirika lako litawasilisha ombi la uteuzi katika tuzo, kumbuka kuwa uteuzi wako lazima uwe umeandaliwa kwa Kiingereza.
Stevie Awards for Great Employers ni programu ya pekee ya tuzo zinazotambua wataalamu wa rasilimali watu na waajiri bora duniani. Shirika la Stevie Awards, ambalo linapeana tuzo, linapatikana Marekani. Wao ni waandaaji wa mashindano nane ya Stevie Awards, ambayo unaweza kujifunza kuhusu kwenye www.StevieAward.com. Kikombe cha ushindi cha Stevie Award kimekuwa mojawapo ya tuzo kubwa zaidi duniani inayotamaniwa.
Katika mwaka wa 2023, Stevie Awards kwa Waajiri Bora (Stevie Awards Great Employers) zilikabidhiwa mashirika na watu kutoka mataifa zaidi ya 28. Bonyeza hapa kuona orodha ya washindi katika awamu ya 2023.
Kuna makundi sita ya tuzo ya kuchagua kwenye Stevie Awards for Great Employers. Ikiwa utahiari kuhudhuria, utachagua makundi ambayo yanaoana na mafanikio ambayo Shirika lako linataka kutambuliwa kwa, na uandae maombi yako ya uteuzi kulingana na maelekezo kwa makundi hayo. Miongoni mwa aina ya makundi yanayopatikana ni kama yafuatayo:
Orodha na maelezo ya makundi yako katika zana ya kuingia.
Katika makundi yote utakuwa na fursa ya kupeana majibu ya maswali kwa kuandika, au video ya urefu wa dakika tano (5) ambayo inajibu maswali hayo.
Tumekusanya orodha ya sababu 10 ambazo shirika lako linapaswa kuwasilisha ombi la uteuzi katika tuzo. Tathmini orodha hapa.
Shirika lolote ulimwenguni linaweza kushiriki. Awamu ya 2024 ya Stevie Awards kwa Waajiri Bora (Stevie Awards for Great Employers) itatambua mafanikio ya mashirika na watu binafsi kutoka Januari 1, 2022.
Kuna tarehe tatu za makataa kwa usajili. Aprili 24 ni tarehe ya makataa ya mapema, kwa ada ya kuingia iliyopunguzwa. Mei 22 ni tarehe ya makataa ya mwisho. Usajili uliochelewa utakubaliwa hadi Juni 26 na malipo ya ada ya kuchelewa.
Uteuzi katika makundi mengi unahitaji malipo ya ada ya kuingia, lakini kuna baadhi ya makundi ambayo unaweza kuingia bila malipo. Malipo yoyote ya kuingia yanayohitajika yameorodheshwa katika zana ya kuingia. Malipo yanapaswa kufanywa kwa Dola za Marekani, aidha kwa kadi ya mkopo, hundi inayotolewa kwa benki ya Marekani, au uhamisho wa pesa kati ya benki.
Stevie Awards zina wawakilishi katika nchi nyingi. Wawakilishi hawa watasambaza habari na kusaidia mashirika katika nchi kushiriki katika tuzo hizo.
Kuamua ikiwa kuna mwakilishi yeyote katika nchi yako, bofya hapa.
Unaweza pia kuwasiliana na waandaaji katika anwani ifuatayo:
Stevie Awards
10560 Main Street, Suite 519
Fairfax, Virginia 22030, USA
Simu: +1 703-547-8389
Faksi: +1 703-991-2397
Barua pepe: help@stevieawards.com
Share